Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC, ameiomba mahakama hiyo kumhukumu kifungo cha gerezani cha miaka tisa hadi 11 mpiganaji wa zamani wa kundi la Ansar Deen, Ahmad al-Faqi al-Mahdi.

Mwendesha mashtaka huyo ameomba adhabu hiyo itolewe kwa al-Mahdi kwakuwa tayari amekiri kuhusika moja kwa moja kwenye uharibifu wa kumbukumbu za kiislam kwenye mji wa Timbuktu mwaka 2015.

Ahmad al-Faqi al-Mahdi amekuwa mpiganaji wa kwanza kutoka Ansar Deen kufikishwa kwenye mahakama hiyo na kusomewa mashtaka na amekuwa mshtakiwa wa kwanza kukiri makosa tangu kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Mahakama hiyo iliyoanzishwa zaidi ya muongo mmoja uliopita ina lengo la kuwashitaki na kuwahukumu wahalifu wa makosa ya kivita.

Ansar Deen waanawatuhumu waislam wanaosalia kwenye nyumba za makumbusho za Timbuktu kuwa ni waabudia makaburi wanaoamini kwenye utakatifu wa watu waliokufa hivyo wamekuwa tishio la imani sahihi ya kiislam hivyo makumbusho hayo yanapaswa kuharibiwa.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *