Staa wa muziki wa Bongo fleva, Mwasiti Alamas amekanusha taarifa zilizoenea kwamba mwanamuziki huyo amepokonywa gari aina ya Benz alilokuwa analitumia hapo awali.

Mwasiti amesema anawashangaa wanaozungumzia maisha yake hususani gari hiyo huku wakiwa hawajui gari lile ni la nani na yeye alikuwa akilitumia kama nani zaidi ya kuongea wanachotaka wao.

Katika hatua nyingine Mwasiti ameeleza kufurahia kupata uongozi mwingine huku akisema kwamba yupo kibiashara zaidi na anaamini kupitia menejimenti hiyo kazi zitakuja nyingi na nzuri kwa kwamba video ya wimbo wake itatoka Januari mwaka 2017.

Mwasiti kwasasa anatamba na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Kaa Nao’ ambao unafanya vizuri katika vituo mba;i mbali vya radio na TV nchini.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *