Baada ya tetesi kuenea mitaani kwamba muimbaji wa Bongo fleva, Mwasiti Almas anachukia mafanikio ya mwanamuziki mwenzake, Vanessa Mdee, mwanamuziki huyo amekanusha taarifa hizo.

Mwasiti amesema kwamba taarifa hizo si za kweli kwani anafurahia mafanikio ya Vanessa kwasababu ni mwanamke mwenzie ila watu wanataka kuwagombanisha.

Vile vile mwanasiti ameongeza kwa kusema kuwa Vanesa Mdee ni rafiki yake mkubwa sana kwa hiyo hawezi kuchukia mafanikio aliyoyapata kwa kwasabu ndiyo imepangwa kuwa hivyo.

Vanessa Mdee
Vanessa Mdee

Mwasiti ambaye alianza muziki muda mrefu kuliko Vanessa Mdee lakini inaonekana kupitwa kifanikio na msanii huyo ambaye ameanza muziki hivi karibuni.

Vannesa Mdee ni mmoja wa wanamuziki wanofanya vizuri nchini pamoja na nje ya nchi kutokana na kushirikiana na wanamuziki mbali mbali kutoka nje jambo ambalo Mwasiti hakuwahi kulifanya hapo nyumba.

Nyimbo iliyompa umaarufu Mwasiti miaka ya nyumba ilijulikana kama ‘Hao’ ambayo alimshirikisha Chid Benz na kufanikiwa kufanya vizuri katika anga ya muziki wa Bongo fleva.

Mwasiti ni mmoja wa wanounda kundi la ‘Sisters’ ambaolo linajishughulisha na harakati za Elimu na Ukombozi kwa mtoto wa kike.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *