Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, Balozi Juma Mwapachu amestaafu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa vipindi viwili.

Mwapachu amechukua uamuzi huo leo baada ya muhula wake wa pili wa miaka mitatu mitatu wa ujumbe wa bodi hiyo kumalizika.

Taarifa iliyotumwa leo na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Acacia imeeleza kuwa inamshukuru Balozi Mwapachu kwa utendaji wake na ushirikiano wake wote  alipokuwa mjumbe.

Kutokana na mabadiliko hayo, Bodi ya Acacia itabaki na wajumbe saba, wakiwamo wanne wakurugenzi na wasio wakurugenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *