Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ameutaka uongozi wa mkoa wa Mwanza kuhakikisha kuwa watu waliopora mali za Chama cha Ushirika cha Nyanza (NCU), wanapatikana na kuzirudisha mali hizo mara moja.

Rais Magufuli amesema NCU kwa sasa inashindwa kujiendesha kutokana na watu wachache kujitwalia mali za NCU kwa kuzinunua kwa bei ya hasara kiasi cha kukifanya chama hicho kutokuwa na uwezo wa kununua mazao ya wakulima.

magufuli 2

Pia Rais alimwambia mkuu wa mkoa wa Mwanza kuwa amezungumza kwamba katika miaka yote aliyepewa Simon Group alikuwa anunue kwa bilioni moja lakini amelipa milioni 30 tu.

Rais Magufuli aliyasema hayo jijini Mwanza wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mkoa huo kwenye Viwanja vya Furahisha vilivyopo Manispaa ya Ilemela.

magufuli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *