Mwandishi wa habari wa KTN kutoka Kenya, Joy Doreen Biira amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa usalama nchini Uganda.

Biira amekamatwa pamoja na wengine watano kwa tuhuma za kupiga picha na video kuhusu operesheni ya maafisa wa usalama katika kasri la mfalme wa Rwenzururu na kuzichapisha kwenye mitandao ya kijamii.

Wanahabari na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wametoa wito kwa serikali kumwachilia huru.

Kauli mbiu ya mwandishi huyo inasema #FreeJoyDoreen imepata umaarufu katika mtandao wa Twitter nchini Kenya.

Wanajeshi na polisi walivamia kasri hilo la Mfalme Charles Wesley Mumbere Jumapili.

Walinzi wake 46 waliuawa kwa mujibu wa polisi, na wengine 139 wakakamatwa.

Mfalme huyo alikamatwa pia na kuzuiliwa makao makuu ya polisi ya wilaya ya Kasese kabla ya kuhamishiwa mjini Kampala.

Gazeti la kibinafsi ya Monitor nchini humo limesema mfalme huyo anatarajiwa kukutana na Rais Yoweri Museveni baadaye leo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *