Mwandishi wa habari mkongwe nchini India, Gauri Lankesh mwenye miaka 55 amefariki dunia kwa kupigwa risasi jana jioni.

Kifo cha Gauri ambaye alikuwa mhariri wa gazeti la kila wiki la Lankesh Patrike, kimetokea katika nyumba yake iliyopo mjini Bangalore.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi la nchini humo, limeripoti kuwa mwandishi huyo ameuawa kwa kupigwa risasi mara mbili kichwani na watu ambao walivamia nyumba yake wakiwa na pikipiki.

Hata hivyo hakuna mtu yoyote ambaye amekamatwa kwa tuhuma za tukio hilo mpaka sasa japokuwa juhudi za upepelezi bado zinafanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *