Mwanamazingira na mwandishi mzoefu mzaliwa wa Italia, Kuki Gallmann amepigwa risasi na kujeuhiwa nchini Kenya na watu wasiojulikana.

Amepigwa risasi ya tumbo akiwa kwenye shamba lake kaunti ya Laikipia nchini humo bila kujua chanzo nii.

Mwezi uliopita magahawa wake wa kifahari uliteketezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji.

Bi Gallmann, amekuwa mwenyeji wa Kenya tangu miaka ya sabini, na anafahamika zaidi kutokana na kitabu chake ‘I Dreamed of Africa’.

Filamu ya kitabu hicho pia ilitolewa, mhusika mkuu, akiwa mwigizaji maarufu wa Marekani , Kim Basinger.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *