Mwanasheria mmoja nchini Uganda Tugume Gideon ameiomba mahakama itoe ruhusa ya kufukuliwa kwa kaburi la aliyekuwa mfanyabaishara maarufu kutoka Uganda , Ivan Semwanga.

Ivan Don alizikwa na kiasi kikubwa cha fedha kilichomwagwa kwenye kaburi lake na waliokuwa rafiki zake wanaofahamika kama ‘Rich Gang.’ siku ya maziko yake.

Pesa zikiwa ndani ya kaburi la Ivan
Pesa zaidi milioni 30 zikiwa ndani ya kaburi la Ivan

Mwanasheria huyo ameiomba Mahakama Kuu ya Uganda kutoa kibali hicho ili fedha hizo ziweze kutolewa kaburini, kwani ni kinyume na sheria kufukia fedha ardhini ambazo ni moja ya nyara za serikali.

Ivan Semwanga alizikwa siku ya Jumanne katika kijiji cha Kayunga nje kidogo ya jiji la Kampala nchini Uganda.

Mfanyabiashara huyo alifariki nchini Afrika Kusini baada ya kupata mshituko wa moyo akiwa nyumbani kwake nchi Afrika Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *