Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Simbu amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza na kushinda mbio ndefu kwa wanaume (marathon) za msimu wa 14 zilizofanyika  jana Mumbai nchini India.

Simbu alifanikiwa kuzishinda  changamoto kutoka kwa mshindi wa pili Joshua Kipkorir wa Kenya ambaye alikuwa anamfuata nyuma kwa muda mrefu.

Simbu alimaliza mbio hizo za kilimita  42.195 kwa muda wa saa 02 dakika 09 sekunde 32 ambapo  Kipkorir alikuwa wa pili kwa muda wa saa 02 dakika 09 sekunde 50.

Baada ya kushinda mbio hizo mwanariadha huyo amesema kuwa mbio hizo zilikuwa ngumu kutokana na washiriki kujipanga zaidi lakini anashukuru mungu.

 

Ushindi wa wanaume na muda waliotumia

1 Alphonce Simbu (TANZANIA) 02:09.32

 

2 Joshua Kipkorir (KENYA) 02:09.50

 

3 Eliud Barngetuny (KENYA) 02:10.39

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *