Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Felix Simbu, leo ataibeba bendera ya Tanzania kwenye  mashindano ya London Marathon yanayofanyika jijini London.

Alphonce ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon.

Kwenye mbio hizo anatarajiwa kuwapa wakati mgumu manguli wa riadha ulimwenguni wanaoshiriki mbio hizo za London akiwemo Muethiopia Kenenisa Bekela pamoja na wengine kutoka Ethiopia na Kenya.

Mwanaradha huyo amesema kuwa “Nitapambana kwa nguvu zangu zote…nina imani nitashinda kwani nimefanya mazoezi ya kutosha na nina ari na moyo wa kushinda”.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Naomba sala za watanzania wote ili niweze kuleta medali nyumbani”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *