Mwanariadha kutoka Kenya, Peres Jepchirchir ameweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za half marathon zilizofanyika Umoja wa Nchi za Kiarabu.

Jepchirchir alimaliza mbio hizo kwa muda wa saa moja, dakika tano na sekunde sita katika mbio za half marathon za Ras al-Khaimah katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Muda wake ulikuwa sekunde tatu bora ukilinganisha na rekodi ya awali iliyowekwa na Mkenya mwingine Florence Kiplagat mjini Barcelona miaka miwili iliyopita.

Rekodi hiyo hata hivyo bado itahitaji kuthibitishwa na shirikisho la riadha duniani kutokana na mbio hizo kutokuwa maarufu sana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *