Mwanamuziki maarufu nchini Malaysia, Wee Meng Chee maarufu kama ‘Namewee’ amekamatwa na polisi baada ya malalamiko kutoka kwa raia kuhusiana na wimbo wake wa hivi karibuni unaokisiwa kuwatusi waislamu.

Mwanamuziki huyo amekamatwa siku ya jana katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia.

Video ya wimbo wake ‘Oh My God’ ambayo inadaiwa kuudhi waisalmu nchini humo, ilizinduliwa Julai ambapo mwanamuziki huyo anaonekana akiimba kwa kutumia mtindo wa kufoka mbele ya msikiti nchini Malaysia.

Mwanamuziki huyo wa mtindo wa rap amesisitiza kwamba wimbo huo wa ‘Oh My God’ una madhumuni ya kukuza maelewano ya kidini miongoni mwa jamii nchini Malaysia.

Namewee-940x580

Polisi nchini humo wamesema wamemkamata na atazuiliwa kwa siku nne kuchunguza iwapo mwanamuziki huyo aliichafua sehemu hiyo ya maombi kimakusudi ili kuitusi dini hiyo.

Kama akipatikana na hatia huenda mwanaumziki huyo akafungwa jela hadi miaka miwili au zaidi.

Robo tatu ya raia wa Malaysia ni Waislamu japokuwa kuna dini kama vile za Kikristo, Kihindu na Kibudha nchini humio.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *