Mmoja wa waanzilishi wa muziki aina ya rock and roll, Chuck Berry amefariki akiwa na umri wa miaka 90 nyumbani kwake katika jimbo la Missouri nchini Marekani.

Muimbaji na mchezaji gitaa huyo alifahamika kote duniani kwa vibao vikali alivyovizindua miaka ya 50s, ukiwemo kibao “Roll Over Beethoven”, ”Sweet Little Sixteen” na “Johnny B. Goode”.

Alianzisha utumiaji wa gitaa wa mchezaji mmoja maarufu kama solos na showmanship kwa wapenzi wa mziki na kuhamasisha mabendi kama vile The Beatles na the Rolling Stones.

Risala za rambi rambi zimekuwa zikimiminika kutoka kwa wanamziki wenzake.

Bruce Springsteen anasema kuwa, Berry alikuwa mtunzi hodari mno wa magoma aina ya rock `n’ roll kuwahi kuishi duniani.

Mick Jagger wa Rolling Stones naye anasema kwamba, ‘aliasha moto wa miaka ya ujanani na kuingiza uhai kwenye ndoto yetu”.

Miezi kadhaa iliyopita, wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa alipofikisha miaka 90, Chuck Berryalitangaza kuzindua kibao kipya, kibao cha kwanza kwa miaka 38

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *