Mwanamuziki wa Marekani, Katy Perry amesema kuwa anataka kumaliza uhasama wake na na mwanamuziki mwenza Taylor Swift.

Kumekuwa na uvumi wa uhasama wa kipindi kirefu kati ya wanamuziki hao wawili na hii ni mara ya kwanza kwa wanamuziki hao kukiri kuwa wana uhasama.

Perry alikuwa katika maonyesho ya James Corden katika kipindi chake cha mazunmgumzo The late late show alipoulizwa kuhusu swala hilo.

Uvumi kuhusu kuwepo kwa uhasama huo ulizuka kabla ya kutolewa kwa kibao kipya cha Taylor Swift Bad Blood.

Amesema katika mahojiano kwamba ni kuhusu mwanamuziki mwengine ambaye amekuwa aduia yake na ni kutokana na biashara.

Siku moja baada ya taarifa hiyo kuchapishwa ,Katy Perry alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter akisema: Mtazameni Regina George aliyevalia nguo za kondoo.

Regina George ni mwigizaji muhimu wa mchezo wa kuchekesha wa Mean Girls unaomuhusisha Lindsey Lohan na Rachel McAdams.

Kulikuwa na uvumi kwamba wanamuziki hao wawili walikuwa wakipigania wachezaji densi nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *