Mwanamke mwenye asili ya Kihindi, Priyanka Yoshikawa ameshinda taji la malkia wa Urembo nchini Japan ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa mtu mwenye asili ya makabila mawili kushinda taji hilo.

Priyanka Yoshikawa mwenye umri wa miaka 22 amesema kuwa atatumia ushindi wake kubadili fikira za watu.

Mwaka uliopita mshindi wa taji hilo Miss Ariana Miyamoto alikuwa wa kwanza mwenye asili yenye makabila mawili tofauti kushinda taji hilo nchini Japan.

Priyanka Yoshikiwa: Akifurahia wakati akitangazwa mshindi wa taji la urembo nchini Japan.
Priyanka Yoshikiwa: Akifurahia wakati akitangazwa mshindi wa taji la urembo nchini Japan.

Ni asilimia 2 ya watoto waliozaliwa nchini Japan ambao huwa wana asili mbili maarufu kama haafua kama wanavyowaita raia wa Japan.

Baada ya ushindi huo Priyanka Yoshikawa amesema kuwa anafurahi kushinda taji hilo na alistahili hilo japokuwa yeye ana asili ya India japokuwa ni Mjapan kwa kuzaliwa.

Ameongeza kwa kusema kuwa baba yake ni Muhindi na anajivunia hilo na anafurahi kwamba ana Uhindi ndani yake lakini hilo halimaanishi kwamba yeye sio Mjapan.

Kutokana na ushindi wa Priyanka Yoshikawa baadhi ya wakosoaji wa mambo wamelalamika kwamba raia mwenye asili ya Japan angefaa kushinda taji hilo la urembo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *