Aliyekuwa mwanajeshi wa Marekani, Robert Harward amekataa kazi ya kuwa mshauri wa masuala ya usalama wa taifa kutokana na kuwa na majukumu mengi ya kifamilia na kifedha.

Mwanajeshi huyo wa zamani alipendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa lakini amekataa kazi hiyo.

Harward alitarajiwa na wengi kuchukua wadhifa huo ulioachwa na Michael Flynn aliyefutwa kazi na Bw Trump Jumatatu.

Flynn alimpotosha makamu wa rais Mike Pence kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi nchini Marekani ambayo aliyafanya kabla yake kuteuliwa rasmi kuwa mashauri.

Pigo hilo kwa Trump la kukataliwa kwa uteuzi wake na Harward, lilitokea saa chache baada ya kutupilia mbali ripoti kwamba utawala wake umekumbwa na mtafaruku mkubwa.

Harward aliambia shirika la habari la Associated Press kwamba utawala wa Trump ulikubali sana kuzingatia mahitaji yangu ya kitaalamu na kibinafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *