Rais wa Marekani, Barack Obama amemwagia sifa Mtanzania Geline Fuko ambaye ni mwanaharakati wa haki za binadamu kwenye hotuba yake katika mkutano wa vijana uliofanyika Washington DC nchini Marekani.

OBAMA 2

Rais Obama amekutana na vijana mbalimbali kutoka bara la Afrika ikiwa ni mpango wa serikali yake kila mwaka kukutana na viajna ambapo alianza kukutana nao toka mwaka 2014 ambao wanaohusika na kuivusha jamii kwenye masuala mbalimbali ikiwemo biashara na siasa.

 Rais Obama alimsifia Geline Fuko kutokana na juhudi zake za kuwawezesha watanzania kusoma katiba ya nchi kupitia simu za mkononi ambapo baadhi ya wananchi wameanza kuijua na kuisoma katiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *