Mwana FA amefunguka na kusema kuwa anatamani sasa kufanya collabo na msanii Christian Bella kwa wasanii wa ndani.

Mwana FA amesema hayo kupitia ‘Account’ yake ya Twitter baada ya kuwapa nafasi mashabiki zake kumuuliza maswali na yeye kuyajibu.

Mbali na hilo Mwana FA amedai kuwa toka ameanza kufanya muziki na kutoa ngoma kibao kali lakini yeye ngoma zake tatu kali anazozikubali zaidi ni pamoja na ‘ Mabinti, Alikufa kwa ngoma, pamoja na Mfalme’.

Wakati ambapo mashabiki wengi walikuwa wanategemea kusikia ‘Remix’ ya ‘Asanteni kwa kuja’, Mwana FA amethibitisha kuwa remix hiyo inakuja muda si mrefu kutoka sasa na kusema kila kitu kimekamilika ila asubiriwa msanii mmoja aingize ‘verse’ yake kwani huyo msanii yupo busy kidogo na mambo yake mengine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *