Mkali wa ‘Dume Suruali’ Khamisi Mwijuma A.K.A Mwana FA amefunguka na kusema kuwa ilimchukua muda sana kupata jina la wimbo huo.

Mwana FA amesema hayo baada ya kukutana na maswali yaliyokuwa yanamsumbua kwa nini wimbo huo aliamua kuupa jina hilo.

Mwanamuziki huyo ambaye aliwahi kuliwakilisha kundi la East Coast Team amesema kuwa baada ya kurekebisha baadhi ya mistari kwenye wimbo huo ndiyo akaamua kumshirikisha Vanessa Mdee kutokana na uimbaji wake na kuupa jina la Dume Suruali.

FA amemaliza kwa kuwataka wasanii wenzake wazingatie mahitaji ya mashabiki ili kuleta muziki mzuri na kupokelewa vizuri katika jamii.

Wimbo wa Dume Suruali umefanya vizuri na unaendelea kufanya vizuri toka utoke mwaka jana ambapo umepata bahati ya kuweka rekodi kwenye mtandao wa Youtube.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *