Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa kitendo cha kuondoka Kocha Mkuu, Hans van Pluijm kimewauma sana lakini hawana budi kusonga mbele na kuhakikisha wanatetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Pluijm amejiuzulu kuifundisha Yanga baada ya uongozi wa timu hiyo kufanya mazungumzo na Kocha mwingine kutoka Zambia, George Lwandamina ili kuchukua nafasi yake pasipo kumshirikisha.

Kufuatia kujiuzulu huko, timu hiyo kwa sasa iko chini ya Mwambusi na wasaidizi wengine waliokuwemo tangu mwanzo hadi uongozi huo utakapoamua hatma yao.

Mwambusi amesema kuondoka kwa Pluijm hakutawafanya kurudi nyuma tayari wamezungumza na wachezaji na kuangalia namna ya kuendelea na mapambano.

Kwa upande mwingine ameomba mashabiki wa Yanga kuendelea kuwaunga mkono ili kutimiza malengo waliyojiwekea.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *