Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa atahakikisha waliomteka Roma na wenzake wanapatikana ili kuzuia matendo hayo maovu.

Mwakyembe amesema kuwa kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania kamwe hawezi kukubaliana na jambo hilo huku akisisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu sana ili aweze kupata majibu ya haraka kabla hajawasilisha bajeti ya wizara yake

Pia Mwakyembe amewataka wananchi waache tabia ya kuamini kila maneno yanayosemwa na watu ambao hawana ujuzi katika masuala ya uchunguzi, hivyo wanapaswa kuvipa muda vyombo vya dola viweze kufanya kazi zake kwa ufasaha.

Mwakyembe ametoa ujumbe kwa vyombe vyote vilivyopo chini ya Wizara yake kutofanya mahojiano yoyote yanayowahusu wasanii hao bila ya kuwepo taarifa kamili kutoka kwake.

Kwa upande mwingine Roma ambaye ambaye amesimulia tukio lilivyokuwa amesema kwa sasa hawezi kuongea mambo mengi kwa kuwa kila kitu amekwisharipoti polisi kila kitu, na kwamba kuna mambo akiyaweka hadharani atakuwa anaingilia upelelezi wa polisi.

Pia amesema hawezi kujua kama kweli tukio hilo lililowatokea  linahusiana na muziki kwa kuwa ameweza kuhusishwa mpaka mfanyakazi wao wa ndani ambaye hana hata chembechembe za uimbaji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *