Wasanii wa Bongo Fleva nchini wametakiwa kuanzisha mfuko wa wasanii kwa ajili ya kutatua changamoto za udhamini zinazowakabili.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe katika kikao na Wasanii hao nchini.

Kikao hicho kilikuwa maarum kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na namna ya kukabiliana nazo hivyo kuwataka kutokata tamaa

Mwakyembe amesema kuwa kutokana na malalamiko na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii, ambazo nyingi zinasababishwa na mikataba inayowanyonya Wasanii katika kazi zao, ni vema sasa Wasanii hao kupitia Chama chao cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) kuanzisha mfuko ambao utakua unatoa mikopo kwa Wasanii ili kuwezesha utendaji wa kazi zao pasipo kutegemea wadhamini.

Mwakyembe amesema kuwa Tasnia ya Sanaa ina mchango mkubwa katika kuongeza pato taifa hivyo ametaka tasnia hiyo kurasimishwa ili kupunguza tatizo la ajira na pia kutumika kama chombo maalumu cha kuielimisha jamii kwani kupitia Sanaa wananchi hupata ujumbe kwa urahisi.

Pia Mwakyembe ameunda Kamati ya kushughulikia masuala yanayowakabili Wasanii ikiwemo sera na sheria ili kuboresha maslahi ya Msanii. Wasanii wanaounda Kamati hiyo ni Azma Mponda, Niki wa Pili pamoja na Witness Mwaijanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *