Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku Runinga na Redio kusoma habari nzima katika magazeti huku akivitaka kusoma vichwa vya habari tu.

Dkt. Mwakyembe ametoa agizo hilo, jijini Mwanza ambapo amesema kutekelezwa kwake kunaanza kesho (Alhamisi) tarehe 04/05.

Leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, Mwakyembe amesema ataendelea kutetea na kulinda haki za waandishi wa habari huku akiwahakikishia ulinzi katika kazi zao.

Mwakyembe amesema amepiga marufuku kusomwa kwa magazeti kwenye runinga na redio, ili magazeti yaweze kuuzwa kwani punde habari yote inaposomwa kwenye chombo cha habari na watu wakasikiliza maeneo yote, hakuna mtu atakayenunua gazeti hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *