Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Harrison Mwakyembe amesema Rais John Magufuli asingekuwa na ujasiri Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ungesainiwa.

Ametahadharisha kuwa sasa Uingereza inaelekea kujitoa EU na tayari Burundi imewekewa vikwazo vya kiuchumi na kwamba mapungufu yako wazi ya mkataba huo.

Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest (Chadema) alishauri wabunge waupitie mkataba na pia upande wa pili wa uzuri wa mkataba huo ujadiliwe na kuchambuliwa na wataalamu kwa Bunge na kushauri nini taifa lifanye kunufaika nao, zaidi ya kubaki kwenye ubaya pekee.

Suala la taifa lifanyeje kutokana na mkataba huo, Mbunge wa Makete, Profesa Norman Sigala (CCM), ameshauri kuwepo na mwongozo kama nchi ifanye nini kuhusu mkataba huo.

Hasa katika suala la uwekezaji wa viwanda kwa bidhaa za nchi ili kutoliumiza Taifa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *