Gazeti la Mawio limefungiwa kwa miaka 2 baada kuandika habari kuhusu marasi wastaafu Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete kwenye sakata la mchanga wa madini (Makanikia).

Barua kutoka kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Harrison Mwakwembe kwenda kwa Mhariri Mkuu wa gazeti hilo inasema kwamba licha gazeti hilo kukiuka maagizo ya serikali lakini pia imekiuka vifungu vinavyokataza uandishi hasi.

Aidha barua hiyo imekanusha Marais tajwa kuhusika na sakata la mchanga na kwamba hawakuwa kwenye sehemu ya uchunguzi ya Kamati za Rais na matokeo ya kamati hizo hayajawatuhumu kwa kosa lolote.

mawio

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *