Aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki ambaye alilazwa kwa ajili ya matibabu nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha wiki moja ameruhusiwa kuondoka hospitalini hapo.

Taarifa kutoka kwa familia yake ilisema kiongozi huyo wa zamani yupo katika hali nzuri kwasasa.

Netcare Sunninghill: Hospitali aliyolazwa rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki nchini Afrika Kusini.
Netcare Sunninghill: Hospitali aliyolazwa rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo ataendelea kukaa nchini Afrika Kusini kwa muda akiendelea kupata nafuu kabla yake kurejea Kenya.

Rais Kibaki alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Netcare Sunninghill kuondoa damu iliyokuwa imeganda kwenye mshipa wa shingoni siku chache baada ya kulazwa.

Wiki moja iliyopita rais huyo wa zamani nchini Kenya alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya matatizo ya kuganda kwa damu kwenye mshipa wake wa shingo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *