Aliyekuwa Rais wa Kenya, Mwai Kibaki amelazwa hospitali nchini Afrika Kusini akipatiwa  matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.

Kiongozi huyo wa zamani nchini Kenya aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi siku ya Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusinihapo jana.

Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu.

Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *