Klabu ya  Mwadui kutoka Shinyanga imemsajili kiungo Awadh Juma kutoka klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.

Uongozi wa Mwadui FC umethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa katika usajili wake wa dirisha dogo, timu hiyo imesajili jumla ya wachezaji wapya 5 wakiwemo wawili kutoka klabu ya Simba.

Katibu Mkuu wa Mwadui FC amesema kuwa klabu hiyo imefuata taratibu zote za usajili na kukubaliana na uongozi wa Simba ambao umetoa baraka na nyaraka zote muhimu za usajili.

Awadhi ambaye alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar, amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza tangu aingie Msimbazi ambapo tangu msimu huu uanze hajacheza mechi hata moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *