Simba SC imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili, golikipa Mwadini Ali na Ame Ali kwa mkopo wa muda mrefu kutoka klabu ya Azam FC.

Wacheza hao wanatarajia kuripoti kambini Jumatatu ijayo mjini Morogoro kuelekea mchezo wa Simba Day Agosti 8, mwaka huu utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba imesajili wachezaji kama Muzamil Yassin, Mohamed Ibrahim, Shizza Kichuya  kutoka Mtibwa Sugar pamoja na Jamal Mnyate kutoka Mwadui FC ya mkaoani Shinyanga.

Simba SC imeweka kambi Mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi ifikapo Agosti 20 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *