Kaya zaidi ya mia moja zimekosa makazi baada nyumba zao kubomoka kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha katika vijiji vitatu vya wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Pia mvua hiyo imesababisha athari kubwa kutokana na ekari za mashamba yenye mazao mbalimbali pia yameathiriwa na mawe yaliambatana na mvua hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya maafa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi, akiwa ameambatana na mwenyekiti wa halmashauri ya Butiama Bw Magina Magesa, wamesema mvua hiyo imesababisha madhara makubwa na kwamba watendaji wa serikali wameanza kufanya tathimini ya kina ili kujua ukubwa wa maafa hayo

Naye diwani wa kata ya Butuguri Bw. Paul Warati, akizungumzia maafa hayo, amesema tathimini ya awali inaonyesha kuwa zaidi ya kaya mia moja,majengo ya taasisi, chakula na mazao mashambani zimeathirika na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *