Wakazi 250 katika kijiji cha Namonge katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, hawana sehemu ya kuishi baada ya nyumba zao kuharibiwa na kuezuliwa mapaa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Diones Minga amesema mvua hizo zimeharibu shule, zahanati pamoja na maghala ya kuhifadhia Chakula ambapo nyumba 47 kati ya 132 zimeezuliwa na upepo mkali.

 

Amesema moja ya sababu ya nyumba hizo kuezuliwa na upepo zinatokana na ujenzi usiokidhi viwango hivyo wameanza kushirikiana na viongozi wa vijiji kuhakikisha nyumba zinazojengwa zinakuwa na ubora wa kuishi kwa ajili ya kuepuka majanga ambayo yanaweza kutokea kama hayajadhibitiwa kwa haraka na wananchi watafute ushauri kabla ya kuanza kujenga nyumba.

 

Naye mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko amesisitiza wakazi wa jimbo hilo kutunza mazingira hasa kwa kupanda miti mingi kwakuwa maeneo mengi yaliyoathiriwa na mvua haina miti kuzunguka eneo husika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *