Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini kuanzia tarehe 25 – 26 Februari mwaka huu kwa ajili ya shughuli za kiserikali.

Museveni anakuja Tanzania kwa mara ya kwanza toka Serikali ya Awamu ya tano chini uongozi wa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli yenye kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu iingie madarakani mwaka 2015.

Mbali na Museveni pia Rais wa visiwa vya Shelisheli, Dany Faure anatarajia kufanya ziara ya siku mbili nchini ambapo anatarajia kuja tarehe 27 – 28 Februari mwaka huu.

Ujio huo wa marais hao umetangazwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusu ugeni huo unaotarajiwa kuwasili nchini ndani ya mwezi huu wa pili.

Makonda amesema kuwa wageni hao watakuwa nchini kwa shughuli mbali mbali za kidiplomasia zinazoguasa nyanja za kiuchumi, Biashara na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *