Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amezua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuwaambia raia wa nchi yake kuwa yeye si mtumishi wao.

Rais Museveni alidai kuwa yeye ni mpigania uhuru na sio mtumishi wa raia wa nchi yake.

‘Sio kiongozi wa zamani au wa sasa katika historia amewahi kuwa mtumishi wa watu. Maneno ‘mtumishi wa watu’ yanatumika kuwahadaa watu. Ni namna ya kukwepa kuzungumza ukweli’.

Mmoja wa wachangiaji wa mtandao ni akasema kuwa:

‘Mpiganaji wa kisiasa anayejipigania mwenyewe na imani zake…Mtu huyu ni ndio tatizo kubwa la Uganda.’

Rais Museveni mwenye miaka 72 aliyazungumza hayo wakati wa hafla ya kusherehekea chama chake cha National Resistance Movement kilipochukua madaraka ya nchi hiyo miaka 31 iliyopita.

‘Mimi ni mpambanaji wa kisiasa, ninayepambana kwaajili yangu na imani zangu. Mimi si mtumishi wa mtu yeyote. Kama kuna anayedhani kuwa amenipa mimi kazi basi anajidanganya mwenyewe. Mimi ni mpigania uhuru ambaye nyinyi mnaamini atawasaidieni pia’

Rais Museveni alishinda uchaguzi uliopingwa na upinzani kwa kuongeza muhula wa tano madarakani mnamo mwezi Februari mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *