Mfanyabiashara wa nguo nchini, Chid Mapenzi ambaye ni mume wa muigizaji nyota wa Bongo Movie, Shamsa Ford ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kujihusisha na  madawa ya kulevya ambao wamo kwenye orodha mpya ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyeitaja leo.

Kufuatia kutajwa kwa jina hilo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa maagizo kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo wa maduka ya Chid Mapenzi yaliyopo hapa jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa Makonda ameyasema hayo kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar ambapo ametangazaza kwamba anayo orodha nyingine ya watu 97 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.

Pia mtu mwingine aliyetajwa ni Ayubu Mfaume ambapo naye anatakiwa kukamatwa haraka iwezekanavyo.

Leo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ametaja majina mengine ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya ikiwa na awamu ya tatu kutajwa kwa amjina hayo ya wanaohusika na uuzwaji wa madawa ya kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *