Kiongozi wa chama kipya cha upinzani nchini Zimbabwe ilichoanzishwa na makamu wa zamani wa rais na aliyekuwa mshirika mkubwa a rais Mugabe, Joice Mujuru, amewafuta uanachama wanachama tisa wa juu wa chama hicho.

Mujuru ambaye alitarajiwa sana kuwa mrithi wa Mugabe alipokuwa Zanu-PF amewafuta uanachama watu hao kwa tuhumaza kuwa vibaraka wa Mugabe ambao wana lengo la kunedelea kumuweka madarakani kiongozi huyo mkongwe zaidi Afrika.

Chama hicho Zimbabwe People First (ZimPF) ambacho kilikuwa kinajumuisha waziri wa zamani wa ulinzi na Didymus Mutasa na msemaji wa zamani wa Zanu-PF Rugare Gumbo.

Lakini chama hicho kimekubwa na mgawanyiko mkubwa tangu mwezi Machi mwaka jana wakati kinaundwa na mgawanyiko zaidi ukatokea baada ya kushindwa uchaguzi na chama tawala cha Zanu-PF mwezi uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *