Muigizaji nyota wa Uingereza, Idris Elba amesema kuwa ataitumia siku ya wapendanao (Valentine Day) kuchangisha fedha za hisani ili kusaidia wasichana wa Afrika.

Kupitia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii amesema kwamba watakaochangisha fedha atawaburudisha katika usiku wa siku ya Valentine ikiwemo vinywaji, chakula na ‘kile mtu atakachopenda.

Amesema fedha za mchango huo zitaelekezwa kwa mashirika ya hisani yanayofanya kazi kuwasaidia wasichana barani Afrika.

Mshindi atajiunga na Elba katika chakula cha jioni cha ‘Candlelit’ katika mkahawa mmoja aupendao .

Usafiri wa ndege, malazi na hoteli yenye hadhi ya nyota nne vitakuwemo kulingana na nyota huyo katika mtandao wake wa Omaze.

Wanaotaka kushiriki wana hadi tarehe 14 mwezi Februari kuwasilisha maombi yao ili kujihakikishia kushiriki.

Elba aliweka sauti katika filamu ya Shere Khan kwa jina Jungle Book pia ametayarisha na kuigiza katika filamu ya Beats of No Nation 2015.

Pia anatarajiwa kuigiza katika filamu ya The Dark Tower mwaka huu filamu ya kutisha itakayoshirikisha msururu wa vipindi vya kitabu cha Stephen King.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *