Muigizaji wa filamu nchini Marekani, Johny Depp amesema kuwa alitishia kumuua rais wa Marekani Donald Trump wakati wa hotuba katika sherehe za Glastonbury.

Je unaweza kumleta Trump hapa? Aliwauliza mashabiki huku akizindua filamu yake ya The Libertine.

Baada ya kuzomewa na mashabiki aliongezea: Hamukuelewa kabisa ni lini muigizaji alimuua rais? Nataka kuweka wazi.

Nyota huyo alikiri kwamba matamshi yake ambayo yanafananishwa na mauaji ya rais Abraham Lincoln yaliotekelezwa na muigizaji John Wilkes Booth 1865 yatazua hisia..

Muigizaji huyo sio wa kwanza kusema kuhusu kumuua rais huyo wa Marekani ambaye anaonekana kupingwa na baadhi ya wasanii nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *