Muigizaji nyota wa Hollywood, Debbie Reynolds amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 siku moja tu baada ya kifo cha binti yake, Carrie Fisher.

Debbie Reynolds alikimbizwa hospital baada ya kushikwa na ugonjwa nyumbani kwa mtoto wake wa kume huko Beverly Hills.

Debbie Reynords akiwa na mwanawe Carrie Fisher ambao wote ni marehemu kwasasa.
Debbie Reynords akiwa na mwanawe Carrie Fisher ambao wote ni marehemu kwasasa.

Muigizaji huyo umaarufu wake ulianza mwaka 1952, wakati alipofanya tamasha sambamba na Gene Kelly katika wimbo uliojulikana kama ”Singin in the Rain.’

Kifo cha muigizaji huyo kimetokea siku moja baada ya kifo cha mtoto wake Carrie Fisher aliyefariki akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kusumbuliwa na shambulio la moyo wakati akiwa kwenye ndege kutoka London kwenda Los Angeles.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *