Muigizaji wa Bongo movie, Daudi Michael maarufu kwa jina la Duma amesema kuwa hana bifu yoyote na muigizaji mwenzie, Gabo Zigamba kama taarifa zinavyoenezwa katika mitandao ya kijamii.

Kauli ya muigizaji hiyo inakuja kufauatia taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wana bifu kutokana na ushindi alioupata Gabo kwenye tuzo ya EATV ambayo walikuwa wote wakiwania tuzo ya muigizaji bora wa kiume.

Duma amesema kwamba yeye na Gabo wapo vizuri sana na hakuna tofauti yoyote ila mashabiki ndiyo wanataka kumgombanisha na muigizaji mwenzie ila hakuna bifu inayoendelea.

Gabo Zigamba
Gabo Zigamba

Muigizaji huyo aliendelea kwa kusema kuwa ushindi wa Gabo ameukubali na asiyependa kushindwa si mshindani kwani baada ya utoaji wa tuzo hizo aliposti taarifa ya ushindi wa Gabo kwenye akaunti yake ya Instagram.

Imekuwa kawaida kwa mashabiki wa Bongo kuwatengenezea bifu wasanii ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika sekta fulani kwa mfano bifu ya Alikiba na Diamond upande wa Bongo fleva ni bifu iliyoanzishwa na mashabiki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *