Mugizaji wa Bongo movie, Mwanaheri Ahmed amesema kuwa anapata wakati mgumu kutokana na baadhi ya watu kumfananisha na staa wa filamu za kibongo Riyama Ally.

Mwanaheri amesema hivi karibuni amekumbwa na dhahama alipokatiza Mtaa wa Kongo, Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya kuchaniwa dera lake kisa kufananishwa na muigizaji huyo.

Muigizaji huyo amesema kwamba amekuwa akikutana na sintofahamu kubwa njiani baada ya watu wengi kumfananisha na Riyama hata kabla ya yeye kuingia kwenye uigizaji wa filamu.

Riyama Ally
Riyama Ally

Mwanaheri amesema ameanza kupata wakati huo mgumu muda mrefu kabla hajaanza kuigiza lakini watu walikuwa wanamfananisha na Rihama Ally ambaye pia ni muigizaji nyota wa filamu za Bongo aliyejizolea sifa miongoni mwa mashabiki wake.

Mwanaheri kwasasa anafanya vizuri na filamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Mwanaheri’ katika soko la filamu za Bongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *