Muigizaji nyota wa Marekani, George Clooney na mke wake ambaye ni mwanasheria maarufu wa haki za binadamu nchini humo, Amal Clooney wanatarajia kupata watoto mapacha mwezi Juni mwaka huu.

Chanzo cha karibu na wawili hao kimesema kuwa ndoa hiyo sasa imekuwa na furaha kutokana na taarifa za kupatikana kwa mapacha hao.

Ndoa ya wiwili hao ilifanyika mwaka 2014 ambapo watu maarufu walihudhuria kwenye harusi hiyo ambao ni Matt Damon na Bill Murray.

george

George Clooney mwenye umri wa miaka 55 ambaye ni muigizaj wa filamu za Hollywood aliwahi kushinda tuzo mbili ambazo ni tuzo za Academy Awards.

Kwa upande wake Mrs Clooney mwenye miaka 39 ni mwanasheria maarufu nchini Marekani ambaye aliwahi kuwawakilisha aliyekuwa waziri mkuu wa Ukrane , Yulia Tymoshenko na muanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange.

Wawili hao wanaungana na familia ya mwanamuziki nyota wa Marekani, Jay Z ambaye anatarajia kupata watoto mapacha na mke wake Beyonce Knowles.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *