Muigizaji wa Marekani, Carrie Fisher amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kukumbwa na shambulio la moyo.

Fisher alikuwa anatoka London kwenda Los Angeles siku ya Ijumaa, Desemba 23 ambapo alipatwa na tatizo hilo la moyo na ikabidi ashushwe kwenye ndege na kupelekwa hospitali ya karibu ambako alipewa matibabu na baadaye kufariki.

Baada ya kuachana na shughuli za filamu za Hollywood mwaka 1973, alijiunga na chuo cha utoaji hotuba na uigizaji cha London, Uingereza, alikokaa kwa mwaka mmoja.

Ujuzi alioupata ndiyo ulimfanya hadi akashiriki filamu maarufu ya ‘Star Wars’ mwaka 1977 akiwa na umri wa miaka 19 tu.

Pamoja na kushiriki filamu hiyo sehemu zote tatu za Star Wars, pamoja na ile ya mwaka jana ya  The Force Awakens,  Fisher alishiriki akiwa nyota katika sinema zilizotoka miaka ya  1980 ambazo ni  The Blues Brothers, The Man with One Red Shoe, Woody Allen’s Hannah and Her Sisters mwaka 1986 na baadaye, When Harry Met Sally.

Fisher amemwacha mama yake aitwaye Reynolds, binti yake Lourd, kaka yake Todd Fisher,  dada wa kambo Joely Fisher na Tricia Leigh Fisher, na mbwa wake mpendwa wa Kifaransa aitwaye Gary.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *