Mugizaji nyota wa Bongo Movie, Ben Branco Selengo amepata ajali mbaya ya gari siku ya sikukuu ya Krisimasi na sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Ndugu wa karibu na muigizaji huyo amesema kuwa ni kweli Ben amepata ajali mbaya ya gari na sasa anapata matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram muigizaji mwenzake Mboto ameandika

Ajali ulioipata sio ndogo kwetu sisi wanadam, lakin kwa mungu ni ndooogo sana. Naamin ndogo kwa mungu kwasababu utapona kwa uwezo wake mungu. Utapona tu inshaallah (Benn Blanco Selengo).

Ajali za barabarani ni janga la kitaifa kwasasa kutokana na uzembe wa madereva ama mwendokasi wa magari.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *