Muigizaji wa Bongo movie, Aisha Bui amefunguka na kusema kuwa bongo movie haitaweza kuendelea kama wasanii wenyewe hawatapendana na kushirikiana wenyewe.

 Muigizaji huyo amesema kuwa kama wasanii hawatakuwa na upendo wowote basi hata kazi zao za sanaa bado hazitaweza kufanikiwa.

 

Pia amesema kuwa wasanii wawe na upendo na wawe na ushirikiano wao wenyewe kwa sababu wameshaichukulia kama kazi na inalipa kodi serikali kupitia hizo hizo filamu.

 

Aidha kuhusu wasanii kutumia kiki katika kazi zao naye alisema kuwa kwa upande wake yeye anaona kama kiki hazisaidii kabisa kwani anaweza kuvuma bila hizo kiki.

 

Muigizaji ni miongoni mwa waigizaji bora wakike wanaofanya vizuri kwenye tasnia kutokana na umahiri wake katika soko la filamu nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *