Muigizaji mkongwe wa Bongo movie, Abdallah Makumbila ‘Muhogo Mchungu’ amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia huku akisema hasumbuliwi hata na mafua.

Muhogo Mchungu amesema kuwa kwa sasa anafanya utaratibu wa kwenda kumshtaki mtu ambaye amesambaza taarifa kwenye mitandao kuwa yeye amefariki dunia.

 

Mbali na hilo Muhogo Mchungu amesema kuwa mitandao ya kijamii ni kama kisu ukiitumia vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii na kuwataka watu wataumie vyema mitandao ya kijamii ili wasilete madhara kwa jamii.

 

Suala ya kusingiziwa kifo kwasasa limekuwa kawaida katika mitandao ya kijamii ukiacha na Muhongo Mchungu wengine waliosingiziwa kifo miaka ya nyuma ni Hadija Kopa na Mwana FA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *