Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewalaumu viongozi wa nchi nyingine za Afrika waliopiga kura ya kupitisha azimio la kuirejesha nchi ya Morocco kwenye Umoja wa Afrika (AU).

Rais Mugabe amesema kitendo hicho kinaonyesha namna ambavyo baadhi ya viongozi wa Afrika walivyokosa itikadi.

Akihutubia kupitia chombo cha habari cha taifa akiwa nchini kwake Zimbabwe baada ya kurejea kutoa Ethiopia kulipokuwa kunafanyika mkutano wa Umoja huo, rais Mugabe alisema kuwa fedha za Morocco ndizo zilizowavutia viongozi wa Afrika na kusahau misingi:

‘Morocco imekuwa ikifanya kazi hapa kwa muda mrefu sana, ikijenga misikiti hapa na kutoa pesa wakati mwingine’

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Herald, Mugabe amedai kuwa hatua ya viongozi wenzake ni pigo kubwa kwa baadhi ya wanachama wa AU.

Mataifa ya Zimbabwe, Afrika Kusni, Namibia na Algeria yanaamini kuwa Morocco ilipaswa kwanza kutangaza kuachana na mpango wa kudai Western Sahara ni sehemu yake na hivyo kuridhia kuwa hiyo ni nchi huru kisha ndipo irudishiwe uanachama wa AU.

Tunaamni katima misngi, kanuni, na tulitaka kuona Morocco ikitangaza wazi angalau, ndio tumeachana na madai kuwa Western Sahara ni sehemu yetu’

Nadhani ni kukosa Itikadi. Wao (Viongozi wa Afrika walioipigia kura Morocco kurudishwa AU) hawana uzoefu wa mapinduzi kama tulionao sisi na wanategemea sana wakoloni wao wa zamani’

Morocco ilijiondoa AU zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *