Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametangaza kuwa raia wote wa nchi hiyo waliokuwa wakituhumiwa kuwaua wazungu waliokuwa wakifanya biashara katika mashamba hawatoshtakiwa.

Akizungumza mbele ya umati wa watu katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Mugabe alisema wazungu hao waliuawa kwa sababu walipinga agizo lililokuwa limewekwa na serikali.

Takribani wazungu 12 waliokuwa wakijihusisha na kilimo katika mashamba ya biashara waliuawa na wanaodaiwa kwamba ni wanaharakati wa Chama cha ZANU-PF na wapiganaji vita wastaafu wakati wakugombea mashamba.

Tukio hilo lilisababisha pia mataifa ya magharibi kumuwekea vizuizi Rais Mugabe asiweze kusafiri kwenda katika nchi hizo wakimtuhumu kwa ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na umiliki mali.

Mugabe amewaambia wajumbe wa mkutano wa mwaka wa ZANU-PF kwamba, hakuna uamuzi wa mahakama utakaobatilisha namna walivyoamua kupata ardhi yao. Alisema kuwa, hata hivyo, ardhi ni yao kwa haki ya kuzaliwa, kama raia ni haki yao, na ni yao kwa kuipigania.

Rais Mugabe amewataka raia wa taifa hilo ambao wamepata ardhi kutokodisha kwa wakulima wakizungu.

Mugabe alisema kwamba taifa hilo halikuwahi kutaka kuwafukuza raia wa kigeni (wazungu) nchini humo na kwamba walioondoka walifanya hivyo kwa maamuzi yao wenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *