Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema kuwa anakubaliana na sera ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba Marekani iwe ya Wamarekani.

Mugabe, ambaye ndiye mara ya kwanza anazungumzia utawala wa Bw Trump, amesema alishangazwa na ushindi wa kiongozi huyo wa Republican.

Hata hivyo, amesema hakutaka pia “Madam Clinton ashinde”, akirejelea mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton.

Mahojiano kamili ya Bw Mugabe yanatarajiwa kupeperushwa rasmi kesho jioni kwenda sambamba na maadhimisho ya kusherehekea kiongozi huyo kutimiza miaka 93 tangu kuzaliwa kwake

Bw Mugabe pia amesema anafaa kuendelea kuongoza, kwani watu wengi nchini mwake wanahisi kwamba hakuna mtu anayetosha kuchukua pahala pake.

Kiongozi huyo tayari ameteuliwa na chama tawala cha Zanu-PF kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *