Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amewalaumu mahakimu wanaoruhusu maandamano dhidi ya serikali ambayo yanandelea nchini humo.

Mugabe amesema mahakimu wanadharau amani, na akawaonya kutothubutu kuonesha dharau wanapofikia uamuzi.

Wafuasi wa upinzani watakwenda mahakamani ili kupinga amri iliyopiga marufuku maandamano kwa majuma mawili.

Kiongozi mmoja wa upinzani, Tendai Biti amemshutumu Rais Mugabe kwamba anajaribu kuwatisha majaji.

Maandamano kadha ya fujo yamefanywa nchini Zimbabwe katika majuma ya karibuni huku msukosuko wa kiuchumi ukizidi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *